Mgombea urais wa muungano wa Azimio La Umoja Raila Odinga, yuko eneo la Pwani kwenye ziara ya siku nne akijipigia debe kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Akihutubu katika kaunti ya Tana River Jumatano Mei 11, Raila aliahidi kushughulikia suala la mafuriko ya mara kwa mara pamoja na kuboresha sekta ya ufugaji. Pia aliahidi kuimarisha kilimo cha unyunyizaji maji mashamba maji, ili kupiga jeki uchumi wa sehemu hiyo.

Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho aliwarai wenyeji wa Pwani, kumpigia kura mgombea rais huyo wa Azimio, akisema ikiwa atachaguliwa ataimarisha bandari za Mombasa na Lamu.

Siku ya Alhamisi, muungano huo wa Azimio utapeleka kampeni zao Kilifi na katika Kaunti ya Kwale siku ya Ijumaa. Mikutano mingine inatarajiwa kuandaliwa katika kaunti ya Mombasa siku ya Jumamosi. Baadhi ya viongozi walioandamana na Raila kwenye ziara yake ya Pwani ni pamoja na kiongozi wa NARC Kenya, Martha Karua, Mwakilishi wa Kike wa Murang’a Sabina Chege, mwaniaji wa ugavana wa Kilifi chini ya muungano wa Azimio La Umoja Gideon Mung’aro, miongoni mwa wagombea wengine.

Source:  https://kiswahili.tuko.co.ke/siasa/454245-raila-odinga-atua-pwani-kwenye-ziara-ya-kisiasa-ya-siku-nne/

Leave a Reply

Your email address will not be published.